Monday, July 17, 2017

WAWKLI WAFA MAJI WAKATI WAKIBATIZWA, JESHJ LA POLISI LAMTIA MBALONI MCHUNGAJI

Watu wawili wamefariki dunia kwa  kuzama katika mto Ungwasi wakati wakiwa kwenye ibada ya ubatizo.

Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro, linawashikilia watu watatu akiwamo mchungaji wa Kanisa la Siloamu wilayani Rombo kwa uchunguzi kwa madai kuwa waumini hao walizama wakati wakiwa katika ibada iliyoandaliwa na kanisa hilo.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamis Issah amesema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana, kwenye mto Ungwasi uliopo Kijiji cha Keni Kata ya Manda chini wilayani hapa.

Issah amewataja waliofariki dunia kuwa ni Gasper Utoh (47) na Proches Mrema (30).

Kamanda amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Huruma kwa uchunguzi zaidi.

Akielezea tukio hilo, Mkuu wa wilaya hiyo Agness Hokororo amesema waumini hao walifariki dunia wakati wakibatizwa.

Sunday, July 16, 2017

Rais Magufuli Ampa pole mwakyembe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe kufuatia kifo cha mkewe Bi. Linah George Mwakyembe kilichotokea usiku wa tarehe 15 Julai, 2017.

Bi. Linah George Mwakyembe amefariki dunia katika hospitali ya Agha Khan Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Katika salamu hizo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho, na amesema yeye na familia yake wanaungana na familia ya Dkt. Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

“Nakupa pole sana Dkt. Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Bi. Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

"Namuombea Marehemu Linah George Mwakyembe apumzishwe mahali pema peponi, Amina” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Waziri KASIM MAJALIWA Asema watanzajia sasa kuachana na nguo za mitumba

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema safari ya Watanzania kuachana na nguo za mitumba imewadia kutokana na uwepo wa viwanda vya kutengeneza nguo nchini.

Pia amesema uwepo wa viwanda hivyo utasaidia wakulima wa pamba kupata soko la uhakika hivyo amewataka walime pamba ya kutosha ili viwanda vipate malighafi.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo   Jumamosi, Julai 15, 2017 wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Namera kilichoko Gongo la Mboto na kiwanda cha nguo cha Nida kilichopo Ubungo Dar Es Salaam.

Alisema viwanda vya kutengeneza nguo nchini ni ushahidi tosha kwamba nchi iko njiani kuondokana na matumizi ya nguo za mitumba kwa kuwa nguo nyingi zitakuwa zinatengenezwa nchini, hivyo kupatikana kwa bei nafuu.

Alisema kwa sasa wanunuzi wa pamba hawana sababu ya kwenda kuuza nje ya nchi na badala yake wauze katika viwanda vya ndani ili vizalishe nguo za kutosha zitakazouzwa nchini kwa gharama nafuu.

“Pamba yote inaweza kuchakatwa nchini, hivyo hakuna haja ya kuiuza nje ya nchi. Natoa wito kwa wakulima wetu wa pamba walime mazao ya kutosha kwa sababu soko la uhakika ipo na hii ndio safari ya mwisho ya mitumba.”

Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha saruji cha Lake kinachozalisha saruji ya nyati ambapo aliwapongeza wawekezaji wote nchini kwa kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuifanya Tanzania kuwa ya uchumi wa viwanda.

Katika kiwanda hicho ambacho kinazalisha tani 700,000 kwa mwaka kimeajiri watu 2000 na kinalipa kodi ya  sh. bilioni 81.312 kwa mwaka, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wake wawe waaminifu, wafanye kazi kwa weledi na wawe waadilifu.

Pia Waziti Mkuu alitoa wito kwa wamiliki wa viwanda vyote nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi waishio katika maeneo ya karibu na viwanda sambamba na kulipa kodi kwa wakati na kwa viwango sahihi.

MWANAHESABU MSOMI RAIA WA IRAN AMEFARKKI UKO NCHINI MAREKANI.

Maryam Mirzakhani, mwanamke wa kwanza kushinda tuzo la hesabu la Fields Medal amefariki nchini Marekani.

Professor Mirzakhan mwenye umri wa miaka 40 ambaye ni professor katika chuo cha Stanford, alikuwa akiugua ugonjwa wa Saratani ya matiti ambayo ilisambaa hadi kwa mifupa yake.

Alipewa jina mshindi wa Nobel ya hesabu. Tuzo la Fields Medal hutolewa baada ya kila miaka minne kwa kati wa wasomi wa hesabu wawili na wanne walio chini ya miaka 40

TAARIFA KWA UMA KUTOKA IDALA YA UHAMIAJI TANZANIA

Idara ya Uhamiaji inapenda kuwakumbusha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi mbalimbali na Wageni wote kuhakikisha wamehakiki vibali vyao kupitia Mfumo wa Uhakiki ambao unapatikana kupitia Tovuti ya Idara ya www.immigration.go.tz kabla ya zoezi la uhakiki kuisha tarehe 19/07/2017.

Kwa wale ambao kumbukumbu za vibali vyao hazitaonekana katika mfumo wa uhakiki au kuwa na tatizo lolote wanashauriwa kuripoti katika Ofisi za Uhamiaji za Mikoa au kwa Mamlaka husika ndani ya muda uliotolewa.

Baada ya kuisha kwa muda uliotolewa, Idara itafanya ukaguzi nchi nzima na kuwachukulia hatua za kisheria Wageni binafsi, Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo wageni wao watabainika kuwa na vibali vya kughushi au vilivyopatikana nje ya utaratibu wa utoaji vibali.

Idara ya Uhamiaji ilitoa muda wa siku 90 kwa wale wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki vibali vyao; tangu tarehe ya kuzindua mfumo huo tarehe 19 Aprili, 2017.

Imetolewa na;

KITENGO CHA UHUSIANO,

MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI

RAIS KAGAME AJITABIRIA USHINDI WA NGUVU RWANDA

Rais wa Rwanda Paul Kagame tayari anadai kuwa mshindi katika uchaguzi ujao wa Rais utakaofanyika tarahe nne mwezi ujao.

Kagame amewaambia wafuasi wake katika mkutano wa kwanza wa kuanza rasmi kwa kampeni nchini humo kuwa matokeo ya uchaguzi tayari yalijulikana mnamo mwaka 2015 wakati Wanyarwanda waliposhiriki katika kura ya maoni ili bunge kuifanyia katiba mageuzi ya kumruhusu kugombea muhula mwingine.

Kagame amesema wapinzani wake hawawezi kubadilisha mapenzi ya wananchi kuwa yeye ndiye chaguo lao.

Paul Kagame licha ya kuwa anasifiwa kwa kuleta uthabiti katika taifa hilo la takriban watu milioni 12, anashutumiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia mkono wa chuma kuliongoza taifa na kuwakandamiza wapinzani