Sunday, July 16, 2017

TAARIFA KWA UMA KUTOKA IDALA YA UHAMIAJI TANZANIA

Idara ya Uhamiaji inapenda kuwakumbusha Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni, Taasisi mbalimbali na Wageni wote kuhakikisha wamehakiki vibali vyao kupitia Mfumo wa Uhakiki ambao unapatikana kupitia Tovuti ya Idara ya www.immigration.go.tz kabla ya zoezi la uhakiki kuisha tarehe 19/07/2017.

Kwa wale ambao kumbukumbu za vibali vyao hazitaonekana katika mfumo wa uhakiki au kuwa na tatizo lolote wanashauriwa kuripoti katika Ofisi za Uhamiaji za Mikoa au kwa Mamlaka husika ndani ya muda uliotolewa.

Baada ya kuisha kwa muda uliotolewa, Idara itafanya ukaguzi nchi nzima na kuwachukulia hatua za kisheria Wageni binafsi, Waajiri, Wakurugenzi wa Makampuni na Taasisi mbalimbali ambazo wageni wao watabainika kuwa na vibali vya kughushi au vilivyopatikana nje ya utaratibu wa utoaji vibali.

Idara ya Uhamiaji ilitoa muda wa siku 90 kwa wale wote wenye vibali vya ukaazi kuhakiki vibali vyao; tangu tarehe ya kuzindua mfumo huo tarehe 19 Aprili, 2017.

Imetolewa na;

KITENGO CHA UHUSIANO,

MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI

No comments:

Post a Comment