Monday, May 15, 2017

Jinsi ya kuzuia na kuondoa chunusi

Wapo watu ambao wanasumbuliwa na tatizo sugu la chunusi, madoa doa na kuharibika kwa ngozi. Ingawa chunusi hizi mara nyingi hutikea usoni, wakati mwingine hutokea pia katika maeneo tofauti ya mwili. Kwa bahati mbaya baadhi ya waathirika wa chunusi wamejikuta wakitumia madawa mengi bila matibabu, hata mara nyingine kuharibu kabisa ngozi zao. Habari njema ni kwamba, imegundulika kwamba matatizo mengi ya ngozi yanayotokea usoni, hasa chunusi ni kwa sababu ya aleji (mzio) ya vyakula tunavyokula, au matatizo mengine yatokanayo na vyakula vya protini. Kwa bahati mbaya, madaktari wengi wa aleji hawawezi kugundua kama chunusi ulizo nazo ni aleji kwa sababu wanafanya allergy test kwenye ngozi, wakati aleji yenyewe iko ndani tena kwenye kiungo specific na yanayoonekana nje ni madhara tu Vyakula mabvyo vimetajwa kuwa huweza kusababisha allergy ni; - Maziwa - nyama - mayai - samaki - kuku - wadudu wanaoliwa kama senene, kumbikumbi nk Hata hivyo sio rahisi kwa mtu mmoja kuwa na allergy ya hivyo vitu hapo juu vyote, na hivyo haimaanishi kama una hilo tatizo basi ndio mwisho wako wa kupata animal protein hapana, ingawa unaweza kuwa na allergy ya kimoja au baadhi ya hivyo. Je, utagunduaje kama chunusi ulizo nazo zinasababishwa na allergy ya kimoja au baadhi ya vitu nilivyotaja hapo juu? Kumbuka, unaweza kutembelea hospitali zote wakafanya allergy tests zote na wasione tatizo, lakini allergy bado iko pale pale. Kwa maana hiyo, namna pekee ni kwa wewe mwenyewe kujifanyia test kama ifuatavyo; 1. Acha kabisa kutumia vyakula vyote vilivyotajwa hapo juu kwa wiki 3. Ina maana kwa wiki hizo 3, utakuwa vegetarian..lol 2. Kama hautaona mabadiliko yeyote, then utagundua kuwa tatizo lako sio allergy hivyo endelea na maisha kama kawaida, huku ukitafuta matibabu mengine. 3. Kama utaona mabadiliko ya kupungua au kuisha kwa tatizo, then mshukuru Mungu wako, maana tatizo lako linaelekea kupata ufumbuzi. Cha kufanya hakikisha tatizo limeisha kabisa ndani ya hizo wiki tatu, au ukiona limepungua halijaisha, then subiri hadi liishe then nenda kwenye step 4 hapo chini... 4. Tatizo likiisha, anza kurudisha kimoja kimoja, ukianza na mayai. Kula mayai 1-2 kila siku kwa siku 7-10 halafu jiangalie kama tatizo lipo. Kama limerudi, acha mara moja kutumia mayai, na subiri hadi liishe kisha ndipo uende step 5 hapa chini 5. Tumia maziwa (kumbuka hii ni siku 10 tangu uanze kutumia mayai). Unaweza kuendelea kutumia mayai (kama hayakuleta tatizo katika step 4), kwa rate ya kawaida uliyokuwa umezoea zamani. Kunywa takribani 200ml hadi 500ml kwa siku kwa siku kumi. Hapa naongelea maziwa ya ng'ombe. Kama unatumia maziwa ya mnyama mwingine, then nayo yawe tested katika step tofauti. 6. Endelea na vyakula vingine vilivyobaki, ukirudisha kimoja kimoja kila baada ya siku kumi, hadi utakapogundua ni kipi kati ya hivyo hapo juu kinachokusababishia tatizo NB; 1. Nyama ya ng'ombe, mbuzi, nguruwe nk ziwe tested tofauti. Nina rafiki yangu anaathiriwa na nyama ya ng'ombe tu sio kitimoto wala mbuzi! 2. Kwa akina dada/mama, tofauti na chakula pia tatizo linaweza kuhusiana na proteins zilizomo kwenye semen za mwanaume/wanaume, na bahati mbaya sana ni kwamba unaweza kuathiriwa na semen ya mwanaume mmoja na sio mwingine! Kivumbi kitakuwa pale unapoathiriwa na semen za mumeo, mbaye kumwambia mtumie condom sio rahisi... Kama tatizo ni hili, hapa inabidi mpime ama kukubali kuishi nalo, au uwe unatumia anti-ellergens kila mnapokutana, lambo ambalo hakuna Dr yeyote duniani atakushauri ufanye. Kama hujaelewa hiyo regime hapo juu, unaweza ukauliza na kupata ufafanuzi mzuri zaidi... 



..Kwa maelezo zaidi piga 0715791042 au 0652943435